1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vitendo vya hujuma vyalenga miundo mbinu ya reli Ufaransa

26 Julai 2024

Mashambulizi kwenye miundo mbinu ya reli Ufaransa kabla ya kuanza kwa michezo ya Olimpiki, yaliyotajwa na waziri mkuu wa nchi hiyo Gabriel Attal kuwa vitendo vya hujuma, yamesababisha vurugu na usumbufu kwa wasafiri.

https://p.dw.com/p/4inCN
Vitendo vilivyoratibiwa vya hujuma vyalenga miundo mbinu ya reli nchini Ufaransa
Vitendo vilivyoratibiwa vya hujuma vyalenga miundo mbinu ya reli nchini UfaransaPicha: Denis Charlet/AFP

Watu wasiojulikana waliweka vifaa vya kulipuka kwenye sehemu mbalimbali za reli wakati wa usiku, hatua ambayo imeongeza hofu kubwa ambayo tayari imekuwepo ya mashambulizi nchini Ufaransa.

Katika ujumbe kupitia mtandao wa kijamii wa X, Attal aliandika kwamba athari za vitendo hivyo ni kubwa mno na kuongeza kuwa idara zao za kijasusi pamoja na za usalama zimetakiwa kuwasaka na kuwaadhibu wahusika wa vitendo hivyo vya uhalifu.

Ufaransa wafungua Olimpiki kwa ushindi, Ukraine waangukia pua

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ya Umma mjini Paris, imetangaza kuwa uchunguzi utaanzishwa dhidi ya tuhuma za kuharibu mali ambayo inahudumia masilahi ya kimsingi ya taifa.