Putin: Nitakuja Korea kaskazini kuimarisha uhusiano wetu
14 Septemba 2023Matangazo
Kulingana na shirika la habari la serikali ya Pyongyang, Kim alitoa mwaliko huo baada ya mazungumzo na Putin katika Jukwaa la Uchumi kwa Mataifa ya Mashariki, mjini Vladivostok.
Jana Jumatano, Kim aliapa kuisadia Moscow kwa kila hali katika vita vyake nchini Ukraine, matamshi yaliyokosolewa vikali na Marekani pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiyataka mataifa hayo kuheshimu maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Soma pia:Rais Putin akubali mwaliko wa Kim Jong Un
Marekani ilisema jana inaufutilia mkutano baina ya wakuu hao wawili kwa karibu na kuionya Korea Kaskazini kwamba itakabiliwa vikali ikiwa itamsaidia Putin.