UchumiChina
Von der Leyen: EU tayari kulinda uchumi wake dhidi ya China
6 Mei 2024Matangazo
Von der Leyen ameyasema hayo mjini Paris kufuatia mazungumzo na Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Kiongozi huyo wa ngazi ya juu ameeleza kwamba bado kuna tofauti baina ya Ulaya na China na ambazo zinazua wasiwasi mkubwa.
"Ili biashara iwe na usawa, ufikiaji wa soko la kila mmoja unapaswa kuwa wa pande zote. Na tumejadili namna ya kupiga hatua za kweli katika kulifikia soko. Bado nina imani kwamba maendeleo makubwa yanaweza kupatikana," amesema Von der Leyen.
Kando na Ufaransa, Rais Xi anatarajiwa pia kuzuru Serbia na Hungary.