1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vurugu zimetanda Jerusalem

Admin.WagnerD6 Oktoba 2015

Hali ya wasiwasi imezidi kutanda na vurugu zikiongezeka Mashariki mwa Jerusalem pamoja na eneo la Ukingo wa Magharibi ingawa hazijafikia kiwango sawa na kile cha makabiliano ya hivi karibuni Israel na Palestina.

https://p.dw.com/p/1GjIQ
Jerusalem Attentat
Picha: picture-alliance/Xinhua/Jini

Jeshi la Israel limezibomoa nyumba za wanamgambo wawili wa Kipalestina na kuzingira thuluthi ya eneo la mji wa Jerusalem leo hii, katika mashambulizi yaliyoamrishwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu baada ya Waisrael wanne kuuliwa katika mashambulizi yaliyofanywa na upande wa Palestina. Nyumba hizo zilizobomolewa zilikuwa ni za Ghassan Abu Jamal na Mohammed Jaabis waliouliwa Novemba mwaka jana baada kuwaua marabbi wanne wa Kisrael na polisi mmoja. Netanyahu ameawaamrisha wanajeshi wa Isarel watumie mkono wa chuma dhidi ya Wapalestina huku machafuko yakiwa yanaongezeka.

"Tumeamua kutumia nguvu za mkono wa chuma dhidi ya ugaidi na dhidi wachochezi. Tumetuma vikosi vinne vya Jeshi la Wananchi la Israel (IDF) ndani ya maeneoa ya Yudea na Samaria, pamoja na maelfu ya polisi mjini Jerusalem. Polisi wataingia ndani kabisa ya vitongoji vya Kiarabu, kitu ambacho hakijawahi kufanyika katika siku za nyuma," alisema Benjamin Netanyahu

Netanjahu vor UN-Vollversammlung
Waziri Mkuu wa Isarel Benjamin NetanyahuPicha: AFP/Getty Images/J. Samad

Halikadhalika kilichokuwa chumba cha Muataz Hijazi kimezingirwa. Humtaz alijaribu oktoba mwaka jana kumuua kwa kutumia bunduki mwanaharakati wa kiyahudi wa mrengo wa kulia, na kumuacha na majeraha pia kimezingiwa . Hata hivyo Hijazi aliuliwa kwa akupigwa risasi na polisi wa Israel.

Waisrael wanne wameuliwa na wengine watatu wamejeruhiwa tangu Alhamisi, na wanaoshutumiwa na mauwaji hayo ni wanamgambo wa Kipalestina. Polisi wa Israel wamewaua kwa kuwapiga risasi wawili wa wauwaji hao. Halikadhalika Wapalestina wawili, mmoja wao akiwa ni kijana wa chini ya miaka ishirini, wameuliwa na wengine 170 wamejeruhiwa katika mapigano na wanajeshi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi tangu Jumapili.

Naye Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ameitisha mkutano wa maafisa wa usalama jana. Kwa mujibu wa Shirika la habari la Palestina la WAFA, Abbas amelitaka baraza la kijeshi pamoja na makamanda wa kijeshi kuwa makini na kuwa na tahadhari na kuwanyima Waistael nafasi ya kuichochea hali ya vurugu iliyopo sasa.

Mwandsihi: Yusra Buwayhid/rtre/afpe

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman