Wafanyabiashara kutoka Tanzania kwenda Kenya kupitia mpaka wa Namanga wamesema wanashindwa kuendelea na biashara kutokana na vuramai ya kisiasa inayoshuhudiwa nchini Kenya. Tanzania huiuzia Kenya karibu tani 72,460 za mahindi kila mwaka huku mahitaji ya mahindi kwa Kenya kwa mwaka yakikadiriwa kuwa tani 600,000. Mwandishi wetu Veronica Natalis kutoka Arusha alituarifu zaidi.