SiasaAsia
Vyama nchini Pakistan vyakubaliana kuunda serikali ya mseto
14 Februari 2024Matangazo
Chama cha waziri mkuu huyo wa zamani, Muslim League PML-N kitaunda serikali kwa kushirikiana na chama cha PPP cha Bilawal Bhutto Zardari, kuunda serikali, pamoja na vyama vingine.
Kwa pamoja vitakuwa na viti vya kutosha bungeni. Hapo awali vyama vya PML-N na PPP vilikuwamo katika mseto uliomwondoa madarakani waziri mkuu Imran Khan mnamo mwaka 2020.
Soma pia:Vyama vya Pakistan vimekubaliana kuhusu muungano
Hata hivyo wagombea huru, waliokiwakilisha chama cha Imran Khan PTI ndio waliopata kura nyingi zaidi katika uchaguzi huo. Nawaz Sharif anapanga kumteua mdogo wake Shehbaz Sharif, kuwa waziri mkuu.