1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SPD, CDU vyapambana na mageuzi ya ajira, uhamiaji

11 Februari 2019

Vyama tawala nchini Ujerumani vinajaribu kuweka kando miwaganyiko ya muda mrefu kuhusu sera za mageuzi ya sekta ya ajira na uhamiaji, lakini matokeo yanaweza kuzusha mzozo mkubwa katika serikali ya muungano.

https://p.dw.com/p/3DAYU
Deutschland | SPD-Klausurtagung Andrea Nahles und Lars Klingbeil
Mwenyekiti wa SPD Andrea Nahles akizungumza katika mkutano wa chama hicho Jumapili, 10.02.2019 mjini Berlin.Picha: picture-alliance/dpa/G. Fischer

Muungano wa Merkel wa vyama vya Christian Democratic Unioni na Christian Social Union unaongoza serikali ya muungano mkuu wa kile kilichokuwa vyama vikuu vya Ujerumani pamoja na chama cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto SPD, kinachojaribu kurudisha nyuma anguko katika maoni ya wapigakura kuelekea uchaguzi wa mwaka huu wa bunge la Ulaya.

Uongozi wa chama cha SPD Jumapili uliidhinisha mapendekezo kadhaa yanayolenga kuyapa nguvu mageuzi ya soko la ajira yalioanzishwa na chama hicho miaka 16 iliyopita, na pia kutoa wito wa nyongeza kubwa katika kima cha chini cha ujira nchini Ujerumani, na haki ya kufanyia kazi nyumbani.

Mageuzi hayo na makato yalioanzishwa waakti wa uongozi wa kansela Gerhard Schroeder yamesifiwa kwa kuimarisha uchumi lakini yaliwatenga wengi wa wapigakura wa chama hicho.

Mwenyekiti wa chama Andrea Nahles alitangaza kuwa Wasosho Democrat "wanatuachia" mfumo wa muda mrefu usiopendwa wamafao wenye mipaka na wa masharti kwa wasio na ajira ulioanzishwa chini ya Schroeder.

Deutschland PK CDU/CSU - Asyl-Streit | Annegret Kramp-Karrenbauer
Mwenyekit wa CDU Annegret Kramp-Karrenbauer.Picha: picture-alliance/Geisler-Fotopress/Snapshot/F. Boillot

Kuna nafasi ndogo ya kufanikisha mfumo huo katika muungano ambao chama cha SPD kilijiunga nao kwa kusitamwaka uliyopita. Naibu kiongozi wa chama cha CDU, Volker Bouffier, alisema kwamba wanachopanga ni kuzika mfumo wa uchumi wa soko la kijamii.

Wasosho demoracat wanatumai kwamba mapendezo kadhaa yanayolemea mrengo wa kushoto yakihusisha pia wito wa kuimarisha pensheni kwa watu wenye kipato cha chini, huenda yakawasadia kuepuka kupata matokeo mabaya kwenye uchaguzi wa bunge la Ulaya, au mapitio ya kati ya muhula yaliokubaliwa tayari kuhusu utendaji wa serikali ya muungano baadae mwaka huu, yanaweza kukilaazimu chama hicho kujitoa katika serikali.

"Tunataka kuongoza, lakini tunataka kuongoza kwa mawazo ambayo yanaendana na wakati," alisema katibu mkuu wa SPD Lars Klingbeil katika mahojiano na kituo cha Televisheni ya umma cha ZDF.

Chama cha CDU kilikuwa kinafanya mkutano wake siku ya Jumatatu, kushughulikia suala muhimu ndani ya chama tangu Merkel aliporuhusu idadi kubwa ya wahamiaji kuingia nchini mwaka 2015 - na kuwakasirisha wahafidhina huku akikisaidia chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD.

Mwenyekiti mpya wa chama Annegret Kramp-Karrenbauer aliitisha mkutano huo baada ya kumrithi Merkel mwezi Desemba, katika juhudi za kuzuwia suala hilo kugeuka zimwi kwa chama hicho, katika namna ambavyo suala la mafao na sera yaajira ilivyogeuka mwiba kwa chama cha SPD. Merkel mwenyewe hakuhudhuria mkutano huo.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/afpe

Mhariri: Josephat Charo