Ufaransa yajiandaa kwa mgmo mkubwa wa wafanyakazi
6 Machi 2023Mgomo huo ni awamu nyingine ya mapambano kati ya serikali ya mrengo wa kati na wapinzani wasiotaka mageuzi ya mfumo wa pensheni, baada ya kushuhudiwa maandamano makubwa mara tano mwaka huu.
Vyama vya wafanyakazi vimeitisha mgomo na maandamano nchi nzima, hatua ambayo Waziri wa Usafiri Clement Beaune, ametahadharisha kwamba itakuwa na athari kubwa sana kote nchini Ufaransa.
"Kutakuwa na athari kubwa sana" kutokana na mgomo huo, Waziri wa Uchukuzi Clement Beaune alisema kwenye shirika la utangazaji la kikanda la France-3 siku ya Jumapili. "Ninajua kuwa kwa watu wengi itakuwa usumbufu mkubwa."
Waziri wa Kazi Olivier Dussopt, akizungumza kwenye shirika la utangazaji la FranceInfo siku ya Jumatatu, alisema "kuonyesha kutokubaliana ni halali, lakini haipaswi kusababisha kuzuia nchi, ambayo itakuwa hatari kwa uchumi wetu."