Waamuzi wa kike katika Kombe la Dunia la FIFA 2022
30 Juni 2022Fainali za Kombe la Dunia kwa wanaume nchini Qatar zitashirikisha waamuzi sita wa kike na wote wamelazimika kukabiliana na hali ngumu.
Mara ya mwisho Neuza Ines Back alikuwa Qatar kwa mchezo, alikuwa sehemu ya timu iliyosimamia fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu la 2020, wakati mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich, walipowafunga wababe wa Mexico Tigres 1-0 huko Al Rayyan.
Akitoka magharibi mwa Brazil, tayari amekuwa mwamuzi wa michezo wa kiwango cha juu katika nchi yake na pia Kombe la Dunia la Wanawake la 2019 nchini Ufaransa. Na Sasa amekuwa mwamuzi msaidizi wa akiba katika hafla ya klabu bora ya FIFA, pamoja na mshirika wake Edina Alves Batistaa akiwa mwamuzi wa nne katika mashindano hayo.
Wasiwasi, uadui na ubinafsi
Katika hafla ya upokeaji medali baada ya mechi, Sheikh Joaan bin Hamad Al Thani, wa familia ya kifalme ya Qatar, walisalimiana kwa kugonga ngumi na wachezaji wa kiume na maafisa wa kiume wakati wakimpita kuchukua medali zao. Lakini Back na Batista walipomfikia, Al Thani alionekana kuwatazama wanawake hao wawili kana kwamba hawapo.
Ingawa sheria ya Kiislamu inakataza wanaume kuwagusa kimwili wanawake nje ya familia zao za karibu, haiwazuii kuwa na adabu kwa kuinamisha macho yao na kufanya ishara nyingine zisizohusiana na kugusana.
Sasa, anatazamiwa kurejea Qatar kama mmoja wa wanawake sita katika timu ya wasimamizi 129 kwenye Kombe la Dunia la Wanaume mnamo Novemba. Atachukua nafasi yake pamoja na wasaidizi wenzake Kathrnyn Nesbitt (Marekani) na Karen Diaz Medina (Mexico), pamoja na waamuzi wakuu Stephanie Frappart (Ufaransa), Yoshimi Yamashita (Japan) na Salima Mukansanga (Rwanda).
Ni mara ya kwanza katika michuano hiyo mikubwa duniani kushirikisha waamuzi wanawake katika nchi hiyo ya mashariki ya kati ikishutumiwa na mashirika ya haki za binadamu kwa kutumia soka kama jukwaa la kuchafua michezo kuleta madai yasiyofaa ya ukiukaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na ubaguzi wa kijinsia.