Nchini Msumbiji hali bado sio shwari, taarifa zinasema waandamanaji wa upinzani wamefunga mipaka kadhaa ukiwemo mpaka wa taifa hilo na Afrika Kusini ikiwa ni muendelezo wa kupinga kile wanachodai kuhujumiwa katika uchaguzi wa Oktoba 9. Vyombo vya ndani Msumbiji vinasema zaidi ya watu 90 wamefariki kutokana na maandamano. Sudi Mnette amezungumza na mwandishi wa habari, Marcos Muledzera.