1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi Syria waitwaa Daraa

7 Desemba 2024

Shirika linalofuatilia vita nchini Syria linasema serikali ya nchi hiyo imepoteza udhibiti wa jimbo na mji muhimu wa kusini, Daraa, ambao ndio chimbuko la vuguvugu la mwaka 2011 dhidi ya utawala wa Rais Bashar Assad.

https://p.dw.com/p/4nrfB
Syria, Hama
Mpiganaji wa vikosi vya waasi katika mji wa Hama nchini Syria.Picha: Ghaith Alsayed/AP Photo/picture alliance

Kwa mujibu wa mkuu wa shirika hilo, Rami Abdel Rahman, waasi wanadhibiti zaidi ya asilimia 90 za jimbo hilo, baada ya vikosi vya serikali kujiondowa.

Kufikia asubuhi ya jana, waasi walikuwa wametwaa kivuuko cha mpaka wa Syria na Jordan, hatua iliyopelekea Jordan kufunga mpaka wake.

Soma zaidi: Maelfu ya watu wakimbia makwao kuelekea mji wa Homs katikati mwa Syria

Daraa ilichukuliwa na vikosi vitiifu kwa Rais Assad mnamo mwaka 2016, lakini waasi waliweza kusalia na silaha zao ndogo ndogo baada ya kufikia makubaliano na serikali mwaka 2018.

Tayari Marekani imewataka raia wake kuondoka nchini Syria mara moja, huku wizara yake ya mambo ya kigeni ikisema hali inazidi kuwa mbaya na isiyotabirika.