Waasi wa M23 wapuuza wito wa Viongozi wa EAC
30 Machi 2023Kama ilivyotakiwa na viongozi hao wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki huko mjini Addis ababa mwezi wa februari,waasi M23 wamekaidi amri hiyo ya kuondoka kwenye maeneo wanayoshikilia na hivi sasa wanaendelea kujiimarisha.
Kundi hilo linaongeza nguvu katika sehemu tofauti za wilaya za rutshuru na masisi ambako wameendelea kuzishambulia ngome za jeshi tiifu kwa serikali.
Watu 5 wauawa katika shambulizi la majambazi mashariki mwa DRC
Hata hivyo, katika miiji ya Kitshanga hali imezidi kuwa mbaya zaidi kutokana na vurugu zinazo shuhudiwa kila kukicha, na raia wengi wana wasiwasi na maisha yao.
Wakati huohuo, siku ya juma tatu waasi hao waliuteka upya mji mdogo wa mweso kilometa 15 magharibi mwa mji wa kitshanga ambamo mapigano makali yalishuhudiwa kati yao na jeshi la congo nakuongeza kishindo kwa wananchi waliolazimika kukimbilia porini.pamoja nakuitumainia serikali kwa upatikanaji wa Amani.
DRC: Mauaji dhidi ya raia yanaendelea licha ya uwepo wa vikosi vya usalama
Huku hayo yakiendelea ,wanajeshi wa UPDF kutoka nchini uganda watarajiwa pia kuwasili wilayani Rutshuru kupitia mji wa bunagana kwenye mpaka kati ya congo na nchi hiyo, ambamo watahudumu chini mwavuli wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki kwakuleta amani mashariki ya congo.
Hata hivyo, hadi mchana huu waasi wa M23 wamezishambulia ngome za jeshi la congo kando na mji wa mweso ambamo milio ya risasi ilianza kusikika tangu asubuhi ya leo alhamisi.
Mwandishi: Benjamin Kasembe