Bunge la Kenya lapiga kura ya kumuondoa madarakani Gachagua
9 Oktoba 2024Baada ya zaidi ya saa saba za majadiliano, wabunge hao walipiga kura kuridhia kumtimua Gachagua huku 44 wakipinga na mmoja akisusia kura hiyo.
Idadi hiyo imefikisha thuluthi mbili ya kura zinazohitajika kisheria ili kupitisha uamuzi wa kumuondoa madarakani naibu huyo wa rais.
Soma pia: Gachagua akanusha madai ya ufisadi na kujilimbikizia mali
Gachagua sasa anasubiri kuijua hatma yake wakati baraza la Senate litakapojadili hoja hiyo na kuipigia kura. Wabunge walianzisha mchakato wa kumtimua Gachagua Oktoba mosi mwezi huu pale 291 walipotia saini hoja ya kumtimua.
Kiongozi huyo alikabiliwa na makosa 11 ya ufisadi, kutumia vibaya madaraka na kukiuka katiba. Hii ni mara ya kwanza kwa naibu wa rais kuondolewa madarakani kwa njia hiyo chini ya katiba mpya ya 2010.