Wabunge Sudan Kusini wamshutumu Kiir kukiuka makubaliano
19 Septemba 2023Matangazo
Serikali ya umoja wa kitaifa kati ya Rais Kiir na mpinzani na makamu wake, Riek Machar, imeshindwa kutekeleza masharti kadhaa ya mkataba wa amani, ikiwemo kuandaa katiba na sheria ya uchaguzi kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwaka ujao.
Soma zaidi: Sudan Kusini kuandaa uchaguzi wa kwanza wa rais 2024
Siku ya Jumatatu (Septemba 2023), wabunge wanaotoka katika chama cha Machar cha Sudan People's Liberation Movement (SPLM) walipinga kupitishwa kwa Sheria ya Kitaifa ya Uchaguzi, wakionya kuwa ingelisababisha uchaguzi usio wa kidemokrasia, usio wa haki na usioaminika.
Wabunge hao walimshutumu Spika wa Bunge, Jemma Nunu Kumba, kwa kushinikiza kura hiyo bila kuwapa haki yao ya kutoa maoni kuhusu suala hilo muhimu.