SiasaAsia
Wabunge wa Korea Kusini wamemuondoa Rais Yoon mamlakani
14 Desemba 2024Matangazo
Upigaji kura umefanyika huku maelfu wakiingia kwenye mitaa ya Seoulkatika maandamano ya wanaomuunga mkono Yoon na wanaompinga, ambaye alifanya jaribio ambalo halikufanikiwa la kuweka sheria ya kijeshi Desemba 3. Kati ya wabunge 300, wabunge 204 wamepiga kura ya kumuondoa rais kwa madai ya uasi, huku 85 wakipiga kura ya kupinga. Watatu hawakupiga kura, huku kura nane zikibatilishwa. Kwa hatua hiyo, Yoon amesimamishwa kazi huku Mahakama ya Kikatiba ya Korea Kusini ikijadili kuhusu kura hiyo. Mahakama ina siku 180 kutoa uamuzi kuhusu mustakabali wa Yoon.