1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge wa Uganda wataka kuondoa ukomo wa urais

13 Septemba 2017

Wabunge wa chama cha tawala cha Rais Yoweri Museveni wa Uganda, National Resistance Movement (NRM), wamekubaliana kuwasilisha bungeni mswada wa kuondoa ukomo wa umri wa rais kutoka kwenye katiba.

https://p.dw.com/p/2jtYt
Janet Museveni  Yoweri Museveni
Picha: picture alliance/dpa/D.Kurokawa

Katiba ya Uganda kwa sasa inamzuia yeyote mwenye zaidi ya umri wa miaka 75 dhidi ya kugombea urais.

Museveni, mwenye umri wa miaka 73, tayari ni mmoja wa viongozi waliotawala kwa muda mrefu zaidi barani Afrika na amekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo mitatu.

Uchaguzi ujao utafanyika mwaka wa 2021.

Mwezi Julai, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Uganda alisema baraza la mawaziri lilipanga kuanzisha sheria sawa na hiyo.

Sheria nyingi za Uganda huwasilishwa bungeni kupitia kwa mawaziri wa serikali.