1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge wa Ujerumani wataka kuipiga marufuku AfD

30 Septemba 2024

Wabunge kadhaa wa Ujerumani kutoka pande zote za kisiasa wanatafakari kuiunga mkono hoja ya uwezekano wa kukipiga marufuku chama cha mrengo mkali wa kulia, AfD.

https://p.dw.com/p/4lFuf
Ujerumani I AFD - Timo Chrupalla na Alice Weidel
Viongozi wa chama cha AfD; Timo Chrupalla na Alice Weidel.Picha: DW

Mahakama ya kikatiba nchini Ujerumani ina mamlaka ya kubainisha iwapo chama cha kisiasa ni tishio kwa demokrasia na kwa utawala wa kisheria na hivyo kuweza kukipiga marufuku.

Hata hivyo, ni wabunge tu wanaoruhusiwa kuiomba mahakama kuanzisha mchakato huo.

Soma zaidi: Wabunge Thuringia wamchagua spika kutoka CDU na kuikataa AfD

Katika siku za karibuni, umekuwapo mjadala nchini Ujerumani juu ya uwezekano wa kuchukua hatua hiyo dhidi ya AfD inayopinga uhamiaji.

Wabunge wanaotaka chama hicho kipigwe marufuku wanapanga kuwasilisha hoja yao bungeni wiki ijayo.

Hata hivyo, wataalamu wametahadharisha kwamba huenda mchakato huo ukawa wa muda mrefu na kwamba hakuna anayejua matokeo yake.