1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachezaji wa Schalke wakubali kupunguziwa mishahara

28 Machi 2020

Wachezaji ya klabu ya kandanda ya Schalke nchini Ujerumani wamekubaliana kutochukua sehemu ya mishhara yao hadi msimu ujao, ili kupunguza athari za kifedha zilizosababishwa na janga la virusi vya corona

https://p.dw.com/p/3a9rb
Bundesliga | FC Bayern München v Schalke 04
Picha: Getty Images/Bongarts/M. Rose

Wachezaji ya klabu ya kandanda ya Schalke nchini Ujerumani wamekubaliana kutochukua sehemu ya mishhara yao hadi msimu ujao, ili kupunguza athari za kifedha zilizosababishwa na janga la virusi vya corona. Taarifa ya klabu hiyo ya ligi kuu ya kandanda Ujerumani - Bundesliga imesema kuwa wachezaji wa timu ya kwanza wamekubaliana na uongozi wa klabu kuwa hawatachukua sehemu ya mishahara yao na marupurupu hadi Juni 30 mwaka huu.

Hatua hiyo itasaidia kuzilinda kazi za karibu wafanyakazi 600 wa Schalke na kuiondolea mzigo wa klabu hiyo wa kulipa gharama ya mamilioni ya euro. Katika wiki za karibuni, wachezaji wa Bayern Munich, Borussia Dortmund, Union Berlin na Werder Bremen walitangaza kupunguziwa mishahara yao kutokana na janga la virusi vya corona.