1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachezaji watajwa katika "Nyaraka za Panama"

4 Aprili 2016

Maafisa kadhaa wa FIFA wanaokabiliwa na tuhuma za rushwa, mkuu wa UEFA aliyesimamishwa kazi kwa muda Michel Platini na nyota wa Barcelona Lionel Messi ni miongoni majina yaliyomo kwenye nyaraka za Panama

https://p.dw.com/p/1IPEJ
Panama Papers
Picha: picture alliance/maxppp

“Nyaraka za Panama” au Panama papers, zinadai kuwa kampuni moja ya kisheria ya jopo la maadili la FIFA ilikuwa na mahusiano ya biashara na watu watatu walioshtakiwa karibuni katika kashfa ya rushwa ya kandanda la kimataifa. Baadhi ya wachezaji pia wametajwa kutumia makampuni ya nje ili kuhifadhi fedha kutokana na matangazo ya kibiashara yanayowahusu.

Ripoti hiyo ni ya uchunguzi wa mwaka mzima wa Jopo la Kimataifa la Wanahabari Wapekuzi ICIJ na gazeti la Ujerumani la Suddeutsche Zeitung na vyombo vingine vya habari. Nyaraka zinaonyesha kuwa kampuni ya kisheria ya Mossack Fonseca, inayomilikuwa na Juan Pedro Damiani, mwanachama wa kamati huru ya maadili ya FIFA, ilizifanyia kazi kampuni za kigeni zinazohusishwa na Euginio Figueredo, makamu wa rais wa zamani wa FIFA ambaye alishtakiwa Marekani kwa tuhuza za rushwa. FIFA imeanzisha uchunguzi kuhusu nyaraka hizo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu