1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachezaji watano wa akiba kuruhusiwa viwanjani

13 Juni 2022

Chama kinachosimamia sheria za mpira – IFAB kimesema kuwa mabadiliko ya kudumu ya wachezaji watano wa akiba yaatanza kutekelezwa katika ligi zote na kuwa mfumo wa kubaini kama mchezaji ameotea unakaribiwa kuzinduliwa

https://p.dw.com/p/4CdgF
Fußball Bayern München | Trainer Julian Nagelsmann mit Kingsley Coman
Picha: Frank Hoermann/Sven Simon/imago images

Chama kinachosimamia sheria za mpira – IFAB kimesema kuwa mabadiliko ya kudumu ya wachezaji watano wa akiba yaatanza kutekelezwa katika ligi zote na kuwa mfumo wa kubaini kama mchezaji ameotea unakaribiwa kuzinduliwa kwa ajili ya Kombe la Dunia Mwaka huu.

Rais wa FIFA Gianni Infantino amesema mabadiliko hayo ya wachezaji wa akiba, ambayo yalianza kutumika baada ya kuzuka janga la corona, yamefuatia uungaji mkono mkubwa kutoka jumuiya yote ya kandanda.

Amesmea baada ya mkutano wa IFAB kuwa watalaamu wataamua kama mfumo wa kubaini kama mchezaji kaotea au la utatumika wakati Kombe la Dunia litaanza Novemba 21.

Mkuu wa marefarii Pierluigi Collina amesema ana matumaini mfumo huo utaanzishwa katika tamasha hilo.

Mfumo huo unayachungunza maeneo 29 ya data kwenye miguu na mikono ya wachezaji na kuchora picha itayotumika na refarii kwenye televisheni za pembeni mwa uwanja. 

Ulifanyiwa majaribio katika Kombe la FIFA la nchi za Kiarabu mwaka jana mjini Doha na Kombe la Klabu Bingwa Duniani Februari.

reuters