1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafadhili wakutana kuisadia Sudan

Carolyne Tsuma5 Aprili 2013

Baada ya muongo mmoja wa vita ni wakati kwa Sudan kujijenga upya. Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameyasema haya kabla ya mkutano wa kimatifa wa kupata uungwaji mkono wa mchakato wa maendeleo wa mabilioni ya dola.

https://p.dw.com/p/18AKf
. Rais wa Sudan Omar al Bashir ahudhuria mkutano Doha
Rais wa Sudan Omar al Bashir ahudhuria mkutano DohaPicha: Reuters

Karibu wajumbe 400 wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya kutoa misaada na wa serikali watakutana mjini Doha Qatar kuanzia Jumapili ili kuidhinisha mpango wa maendeleo. Wakereketwa wana wasiwasi kuwa msukosuko magharibi mwa kanda ya Sudan huenda ukaathiri juhudi hizo na wafadhili pia wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na vikwazo dhidi ya Sudan.

Mkutano huo umeitishwa kutokana na makubaliano ya amani mwezi Julai mwaka 2011ambapo Sudan ilitia saini makubaliano na muungano wa makundi ya waasi mjini Doha. Makundi makuu ya waasi yalitupilia mbali mkataba huo ambao katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon mnamo mwezi Januari alisema umepiga hatua kidogo katika utekelezwaji wake.

Rasimu ya kurasa 155 kuhusu Sudan inasema kuchelewa kutekeleza mpango huo wa maendeleo utafanya hali ya kujiendeleza ngumu zaidi na kusema hakutakuwa na masharti muafaka wa kuyatekekelza hayo huku ikitafuta dola bilioni 7.2 katika kipindi cha miaka sita ili kujiondoa kutoka kutegemea vyakula vya misaada na mahitaj mengine.

Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa
Shirika la maendeleo la Umoja wa MataifaPicha: APGraphics

Matatizo ya Sudan hayatatuliwi na misaada peke

Jörg Kühnel afisa wa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP anasema chimbuko la mzozo wa Sudan haliwezi kushughulikiwa kwa misaada pekee bali kuwasaidia watu wa Sudan kuyajenga tena maisha yao na kujietegemea.

Mpango huo unanuia kuanzisha msingi wa miradi ya maedeleo ya kudumu Darfur kupitia kuboresha miradi ya maji,barabara na miundo mbinu.Pia inalenga kuboresha kilimo,kutaoa fursa ya kukopa fedha na mbinu nyingine kuwapa wasudan uwezo wa kujitegemea chini ya mfumo bora wa serikali za utawala.

Mkutano huo wa Doha unaitishwa miaka kumi baada ya kuzuka uasi miongoni mwa makundi ya kikabila ya kiarabu.Waasi walitaka kumaliza kile walichokiita kutawaliwa kwa muda mrefu na mabwenyenye wa kiarabu nchini humo.Na kujibu uasi huo,kundi la waasi laJanjaweed lililoungwa mkono na serikali liliushutua ulimwengu kwa ukatili uliofanya dhidi ya raia.

***Trotz Hybrid eine "Mission Impossible" - Die Schwierigkeiten der UN-AU-Hybridmission in Darfur, Scholz*** Activists paint a sign to call attention to the crisis in Darfur, marking the fifth anniversary of the crisis, outside the White House, Sunday, April 13, 2008 in Washington. (AP Photo/William B. Plowman)
UN AU Hybridmission in DarfurPicha: AP

Sehemu kubwa ya Sudan ni tulivu

Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita ICC ilitoa kibali cha kukamatwa kwa Rais wa Sudan Omar al Bashir kwa madai ya kuhusika katika uhalifu wa kivita,uhalifu dhidi ya binadaamu na mauaji ya halaiki.

Licha ya kuwa vita hivyo vimetulia,makabiliano ya kiukoo kati ya waasi na vikosi vya serikali,utekaji nyara na maovu mengine bado vinaendelea.

Maeneo mengi hata hivyo nchini Sudan yamerejesha udhabiti na hivyo basi kutoa fursa ya kujiendeleza na ndiyo lengo kuu la mkutano huo wa Doha unaonuia kupata idhini ya kisiasa ili kutekeleza mpango huo wa maendeleo.

Balozi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Sudan Tomas Ulicny amesema watatangaza ahadi mpya ya usaidizi kwa Darfur huku Marekani ikisema haitaongeza ufadhili wake kwani serikali ya Sudan inapaswa kwanza kutimiza ahadi zake za kifedha na kisiasa chini ya mkataba wa amani.Serikali ya Sudan inahitaji kutoa asilimia 36 ya ufadhili mzima na imesema imeweza kupata dola milioni 200.

Mwandishi: Caro Robi/afp

Mhariri: Hamidou Oummilkheir