Wafanya biashara wa Afrika na Ulaya kuwahimiza viongozi 'wawipige jeki'
7 Desemba 2007Mkutano wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika unaaza kesho katika jiji kuu la Ureno la Lisbon.
Mkutano huu ndio wa kwanza wa aina hiyo kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka saba.Na wakati jiji hilo likijiandaa kuwasili kwa viongozi wapatao 80 kutoka Ulaya na Afrika kwa ajili ya mkutano wa kesho,jana ulifunguliwa mkutano wa kile kinachoweza kuitwa -jukwaa la Afrika la fedha na uwekezaji.
Ripoti kuhusu jukwaa hilo, ilioandaliwa na Alison Roberts akiwa Lisbon .
Lengo la jukwaa hilo limeelezwa kama kutafuta njia za kuisaidia sekta ya kibnafsi kutoa mchango ambao viongozi katika muswada jaribio wao wa pamoja,wanasema wanautaka uchangie.
Calvin Miller kutoka mpango wa chakula Duniani FAO mjini Roma asema kuwa katika jukwa hilo lengo sio kujadilia kukuza biashara ya kilimo katika eneo la Darfur,’kuna athari zake katika baadhi ya sehemu.Na kwa upnde mwingine kuna biashara nyingi zinaingia,kam vile mafuta pamoja na vitu vingine tofauti,kwa hivyo tunajiuliza ni vipi tutakavyoweza kuvishughulikia,
amesema Miller.Na hapo ametoa mfano wa Sudan kama mfano ambapo wawekezaji wa kigeni wanaipuuza nchi ambayo eneo kubwa ni tulivu tena likiwa na sekta tele zinazoweza kuwekezwa.Hata hivyo baadhi ya kampuni zinafuata mada ndogo ya jukwa hilo ya, 'kufufua utajiri wa Afrika'.Kampuni ya Info Terra Limited, tawi la kampuni tanzu ya Uingerza ya European aerospace corporation EADS, inajihusisha kutafuta na kushughulikia habari za kijografia ikitumia mitambo ya Setilaiti na njia zingine.Pia ina miradi mbalimbali nchini Angola. Simon Ashby anasema ardhi kwa ajili ya kilimo, uchimbaji wa madini pamoja na ujenzi wa nyumba ni miongoni mwa sekta ambazo hazijawekezwa vilivyo barani Afika. Anaongeza kuwa sababu kuu ni uhaba wa habari muhimu kuzihusu..Mfano kusajili ardhi.Ni wafrika wachache walio na hati za kumiliki ardhi na kumekuwa na juhudi katika mashirika makubwa kama vile Benki ya Dunia na Umoja wa Ulaya kujaribu kutafuta njia za kumaliza tatizo hilo.Tumeshuhudia uwakilishi mdogo katika mifumo ya unyunyuziaji.Hiyo ni sawa lakini,nikiambiwa kuwekeza hata dola mia katika mfumo huo...naona shida kutokana na athari zake. Nchi kama vile Angola zinaanzia mwanzo lakini zina uchu wa kusonga mbele.Hata hivyo ni safari ndefu kwani unazungumzia miaka 25 hadi 30 kuweza kupata ufumbuzi wa suala la ardhi,
amesema Ashby.
Jose Amaro Tati, ni Gavana wa mkoa wa Bie unaopatikana katikati ya Angola ambako kampuni ya Info Terra inapiga ramani maeneo muafaka kwa kilimo pamoja na ujenzi wa nyumba.Anasema kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini mwake,karibu barabara zote zillkuwa hazipitiki kw minajili ya biashara au uwekezaji hadi hivi majuzi.
Anasema kuwa mataifa mengi barani Afrika yalikuwa maarufu kwa matokeo mabaya. Yeye Edith Miller, Meneja Mkurugenzi wa shirika la kujitolea la EMRC, lililoandaa mkutano au jukwaa la mjini lisbon anasema kuwa ingawa kwa sasa sekta ya kibanafsi ndio wimbo unaosika kote,ili kufanikisha maendeleo, lakini baado kuna mikingamo mingi inayohitaji kuepukwa kwanza.
‚…kuna kutoaminiana katika biashara kati yamabara ya Ulaya na Afrika.Ndio maana ukitaka kumletaUlaya mfanya biashara wa Afrika ni lazima kwanza upate Visa na hawataki kutoa visa hizo.Kwa hivyo unakumbana na matatizo mengi ambayo watu wa bara la ulaya hawa hawayaoni kama matatizo.Na hii ndio maana tume ya Ulaya inashindwa kila mara,
asema Edith Miller.
Wajumbe wa wafanya biashara kutoka Ulaya na Afrika katika jukwaa hilo wamekubaliana kuwa kile kilichoitwa mbegu za mtaji ni muhimu sana ikiwa sekta ya kibnafsi itatoa mchango ambao serikai zinasema zinataka iutoe.Wanasema watawajulisha viongozi wa mkutano wa hapo kesho kuhusu hilo na mengine kupitia tamko la pamoja baada ya kikao chao cha leo.