Nchini Tanzania,wafanyabiashara katika soko la kimataifa la Kariakoo, jijini Dar es Salaam, leo wameanza rasmi mgomo wakiishinikiza serikali kuja na majibu ya kero zao, ikiwamo utitiri wa kodi, biashara ndogo za wazawa kufanywa na wageni pamoja na usumbufu unaodaiwa kufanywa na watendaji wa mamlaka ya ukusanyaji wa mapato Tanzania, (TRA). Sikiliza ripoti ya Florence Majani,