Wafanyakazi 7 wauwawa kusini magharibi mwa Pakistan
30 Septemba 2024Polisi nchini Pakistan wamesema wafanyakazi saba wa vibarua wamepigwa risasi na kuuliwa kusini magharibi mwa nchi hiyo, eneo ambako machafuko ya kikabila yanafanywa na wanamgambo.
Wafanyakazi hao waliokuwa wamehamia mkoa wa Balochistan kwenda kufanya kazi kutokea mkoa wa Punjab, walishambuliwa katika wilaya ya Pangur wakati wa usiku.
Kamanda wa jeshi la polisi la Balochistan lenye makao yake katika mji mkuu, Quetta, Moazzam Jah Ansari, amethibitisha wafanyakazi hao saba wameuwawa na mwingine mmoja kujeruhiwa.
Balochistan ndio mkoa masikini kabisa wa Pakistan licha ya kuwa na raslimali nyingi ambazi bado hazijaanza kutumiwa, ambako makundi ya wapiganaji wanaopigania kujitenga wamekuwa wakiwashambulia maafisa wa ulinzi pamoja na raia wa Pakistan kutoka mikoa jirani.