1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi wa uwanja wa ndege Kenya wasitisha mgomo

1 Septemba 2024

Chama cha wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenya,kimesema mgomo wa wafanyazi uliokuwa umepangwa kufanyika kesho Jumatatu.

https://p.dw.com/p/4k9LH
 Nairobi JKIA
Abiria wanaonekana wakisubiri kwenye foleni ndefu nje ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Novemba 07, 2022. Picha: Billy Mutai/AA/picture alliance

Kwa mara nyingine umeakhirishwa ili kutowa nafasi ya kufanyika mazungumzo. Mgomo huo umeakhirishwa kwa siku saba.

Wafanyakazi 10,000 wa chama wa muungano wa shirika la safari za anga Kenya,wanapinga mipango ya serikali ya nchi hiyo ya kutaka kuingia makubaliano ya uwekezaji na kampuni ya India ya Adani kutanua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta,na kuipa mamlaka ya usimamizi wa uwanja huo.

Chama cha muungano huo wa wafanyakazi wa JKIA pia kimeitaka serikali kiizuie kampuni hiyo ya India kuchukuwa hisa na kufuta mara moja safari ya kuelekea India kesho Jumatatu, ujumbe wa viongozi wa serikali na wasimamizi wa Uwanja huo wa ndege. Wafanyakazi hao wamesema ikiwa serikali itakiuka masharti hayo,mgomo wao utaanza mara moja.