1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Wafanyakazi wa MONUSCO washambuliwa mjini Kinshasa

11 Februari 2024

Mkuu wa ujumbe wa amani nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, Bintou Keita, amesema wafanyakazi wake na magari ya ujumbe huo yameshambuliwa katika mji mkuu Kinshasa hapo jana.

https://p.dw.com/p/4cGhR
Kongo| Bintou Keita.
Mkuu wa ujumbe wa amani nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, Bintou Keita.Picha: Bianca Otero/ZUMA Wire/IMAGO

Shirika la habari la reuters limeripoti kuwa makundi ya watu waliokuwa kwenye pikipiki yalikusanyika katika wilaya ya Gombe, makao ya ujumbe huo unaojulikana kama MONUSCO pamoja na balozi nyingine nyingi.

Katika ujumbe aliochapisha katika mtandao wa kijamii, Keita amesema kuwa magari kadhaa ya ujumbe huo yaliteketezwa.

Ubalozi wa Ivory Coast pia umesema kuwa gari lake moja limeharibiwa mjini Kinshasa, na kutaja kuweko kwa mashambulizi ya kiholela dhidi ya magari ya balozi na mashirika ya kimataifa.

Hata hivyo polisi na serikali ya Kinshasa hazikutoa tamko kuhusu matukio hayo.