1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi wa sekta za rejareja na jumla Ujerumani wagoma

25 Novemba 2023

Chama cha wafanyakazi Ujerumani - Verdi kiliwataka wafanyakazi 10,000 kusalia majumbani na katika jimbo kubwa kabisa nchini Ujerumani la North Rhine Westphalia.

https://p.dw.com/p/4ZRAv
Mamilioni ya wafanyakazi wameathirika na mazungumzo ya nyongeza ya mishahara
Mamilioni ya wafanyakazi wameathirika na mazungumzo ya nyongeza ya mishaharaPicha: Arne Dedert/dpa/picture-alliance

Maelfu ya wafanyakazi wa biashara ya rejareja na ya jumla nchini Ujerumani walifanya mgomo jana Ijumaa, baada ya kukwama kwa mazungumzo ya mishahara.

Chama cha wafanyakazi Ujerumani - Verdi kiliwataka wafanyakazi 10,000 kusalia majumbani na katika jimbo kubwa kabisa nchini Ujerumani la North Rhine Westphalia, karibu watu 3,000 waliitikia wito huo.

Katika mji mkuu Berlin na mji jirani wa Brandenburg, watu 1,350 walifanya mgomo. Chama hicho pia kiliwataka wafanyakazi katika majimbo ya Baden-Wüttemberg, Hesse, Hamburg na Bavaria kugoma.

Mamilioni ya wafanyakazi wameathirika na mazungumzo ya nyongeza ya mishahara.