1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfaransa

Wafaransa kuandamana dhidi ya mabadiliko ya pensheni

13 Aprili 2023

Vyama vya wafanyakazi Ufaransa vinapanga maandamano mapya ya nchi nzima leo kuelekea uamuzi wa mahakama ya kikatiba hapo kesho wanaotarajia utausimamisha mpango wa pensheni wa Rais Emmanuel Macron, unaopingwa pakubwa.

https://p.dw.com/p/4PzSl
Frankreich, Paris | Streiks und Proteste gegen die Rentenreform
Picha: Raphael Lafargue/abaca/picture alliance

Mamia kwa maelfu ya watu wanatarajiwa kujitokeza mitaani kote nchini humo, kwani polisi inatarajia kati ya watu laki nne hadi laki sita washiriki maandamano hayo.

Idadi hiyo itakuwa ni chache ikilinganishwa na watu milioni 1.3 walioshiriki maandamano hayo mnamo mwezi Machi. Iwapo Baraza hilo la Kikatiba litapitisha mabadiliko hayo, mswada huo unaoongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64 huenda ukawa sheria.

Soma pia:Maandamano yaendelea Ufaransa kupinga mpango wa mageuzi ya pensheni

Baraza hilo pia lina uwezo wa kuyakataa baadhi au kikamilifu mabadiliko hayo yaliyopendekezwa na serikali. Dhima ya Baraza hilo ni kuhakikisha kwamba sheria imefuatwa kabla kuipitisha sheria hiyo.