1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia

Oumilkher Hamidou16 Desemba 2008

Mkuu wa polisi ya Passau katika jimbo la kusini la Bavaria ,nusra apoteze maisha katika shambulio linalodhaniwa limefanywa na vichwa upara wenye chuki dhidi ya wageni

https://p.dw.com/p/GH3f
Mkuu wa polisi ya Passau,Alois MannichlPicha: AP


Mkuu wa polisi katika mji wa kusini mwa Ujerumani wa Passau amechomwa kisu jumamosi iliyopita.Wafuasi wa siasa kali ya mrengo wa kulia wanatuhumiwa kua nyuma ya shambulio hilo.Hakuna ushahidi lakini wa dhana hiyo.Na hata waliofanya kitendo hicho bado hawajakamatwa.Kimoja lakini ni dhahir hadi sasa nacho ni kwamba jamii itabidi iwe macho zaidi ikiwa kweli shambulio hilo limeshawishiwa kisiasa.


Fadhaa na mshtuko ni mkubwa kupita kiasi kufuatia shambulio la kutaka kumuuwa mkuu wa polisi ya Passau.Watu wameshtuka kwasababu kwa muda sasa  wamekua wakiamini visa kama hivyo vimepungua .Hakuna aliyekua akitaharuki na kuwakilishwa waafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia katika baadhi ya mabunge ya majimbo.Mikutano ya wanazi mambo leo kama inafanyika,lakini inakua mahala ambako hata jamii haina habari .Na vishindo vya watu wanaovalia buti na makoti meusi yanayotuna,watu vikiangaliwa na kutajwa kua vishindo vya wasiokua na lao,waliotengwa na jamii,wanaokutikana,hakuna ajuae wapi,katika mikoa ya mashariki ya Ujerumani.


Watu walijishughulisha zaidi na mada za kawaida za kisiasa.Na kipa umbele katika mada hizo,hata humu nchini Ujerumani ni mapambano dhidi ya visa vya kigaidi vya wafuasi wa itikadi kali ya dini ya kiislam.Vituko vya wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia vinakosolewa tuu vinapotokea.Lakini havikua tena vikiangaliwa kama kitisho cha kweli katika jamii.


Umwagaji damu wa Passau unatubainishia ukweli kwamba kujaribu kufifiisha mambo lilikua kosa.Kisa cha Passau kinatudhihirishia pia kipeo cha aina mpya cha kadhia hiyo.Tumeshuhudia jinsi mkuu wa polisi alivyoshambuliwa hadharani,kisa,kwasababu ya kuvivalia njuga visa vya chuki dhidi ya wageni.Shambulio hilo linatisha na linatufanya tugutuke.


Madai ya zamani yameingia upya midomoni;hatua kali za kisheria zichukuliwe, watoto wapatiwe mafunzo ya kisiasa, na ya maadili shuleni pamoja pia na jamii kuwa na moyo wa kiijasiri.Yote hayo ni sawa lakini wakati huo huo yanaonyesha watu wameishiwa.


Nini cha kufanya ikiwa jamii imepotelewa na imani kwa taasisi zake?Na kama watu wamepoteza imani ,hasa katika maeneo ya mashariki,kuelekea mfumo wa kidemokrasi?Katika wakati ambapo vyama mfano wa NPD vinazidi kueneza propaganda zao?


Tunashindwa pia kutambua kwamba siasa kali za mrengo wa kulia sio tena suala la kundi dogo la jamii,linanyemelea hadi nyanda za kati za jamii.Wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia wanakutana bila ya hofu naiwe katika mashamba ya matajiri au katika makasri ya fahari.Katika nchi nyingi za Ulaya,kuanzia Ubeligiji hadi kufikia Ufaransa na Austria,wafuasi wa mrengo wa kulia wamegeuka kua sehemu ya wenye usemi katika majukwaa ya kijamii na kisiasa pia.


Na enzi hizi za shida ya kiuchumi ndizo zinazozidi kupalilia uwanja wa siasa kali za mrengo wa kulia.


La maana ni kuchanganya kila aina ya hatua,za kisiasa,kielimu,kisheria na kijamii na muhumi zaidi ya yote ni kwa watu kuwajibika zaidi.







►◄