1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya kupinga kuachiwa kwa Khan yafanyika Pakistan

15 Mei 2023

Misafara ya mabasi na magari yaliyojaa wafuasi wanayoiunga mkono serikali imefurika kwenye barabara kuu inayoelekea mji mkuu Islamabad kupinga kuachiliwa kwa waziri mkuu wa zamani, Imran Khan.

https://p.dw.com/p/4RMNx
Pakistan | Protest Islamabad
Picha: Anjum Naveed/AP Photo/picture alliance

Maelfu ya wafuasi hao wa serikali wanaelekea katika majengo ya Mahakama ya Juu nchini humo katika tukio la nadra la kupinga uamuzi wa kuachiwa huru Khan, ambaye sasa ni kiongozi wa upinzani. Wafuasi hao wameonesha kutoridishwa na kupewa "ahueni isiyofaa" kwa kiongozi huyo baada ya kukamatwa kutokana na tuhuma za ufisadi.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 70 aliachiliwa kwa dhamana na kupewa kinga ya kutokamatwa hadi baadaye mwezi huu.

Hatua ya wafuasi hao ni ishara ya kuongezeka kwa mvutano kati ya idara ya mahakama na serikali ya Waziri Mkuu Shahbaz Shariff, aliyechukua nafasi ya Khan baada ya kuondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye bungeni Aprili, mwaka 2022.