1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagombea urais Tunisia walalamikia vitisho

2 Agosti 2024

Vyama vya upinzani Tunisia, wagombea urais na mashirika ya kutetea haki za binadamu leo yamezituhumu mamlaka kwa vitisho na vikwazo ili kuhakikisha kwamba Rais Kais Saied anachaguliwa tena katika uchaguzi wa Oktoba 6.

https://p.dw.com/p/4j2zr
Tunisia | Rais Kais Said
Rais wa Tunia, Kais Saied akipokea katika Ikulu ya Carthage, Rais wa Algeria Abdelmajid Teboune.Picha: Chokri Mahjoub/ZUMA Wire/IMAGO

Huku muda wa mwisho wa  kujiandikisha katika kinyang'anyiro cha kugombea urais ukikaribia hapo Agosti 6, wanasiasa 11 wa upinzani wanaotarajia kushindana na Saied, wametoa taarifa ya pamoja wakizilaani mamlaka nchini humo. Kati ya wagombea hao 11, hakuna hata mmoja kati yao ambaye amepokea cheti cha kuonyesha kwamba hawajahusika katika uhalifu wa aina yoyote ile, hilo likiwa ni sharti jipya litakalowapa fursa ya kusonga mbele katika hatua ya kujisajili. Msemaji wa tume ya uchaguzi nchini humo amesema wizara ya usalama wa ndani itawasiliana na wagombea hao na kuwapa vyeti hivyo ingawa hakusema ni lini hilo litakapofanyika. Saied alitaganza Julai 19 kwamba atawania muhula mwengine wa urais.