1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagombea wa upinzani Kongo walalamikia dosari za uchaguzi

20 Desemba 2023

Wagombea wakuu wa upinzani katika uchaguzi wa rais unaofanyika leo nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamesema raia wengi wameshuhudia mparaganyiko na dosari nyingi vituoni walipokwenda kupiga kura.

https://p.dw.com/p/4aPgM
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo | Kituo cha kura Kinshasa
Kituo cha kupigia kura mjini Kinshasa.Picha: Dai Kurokawa/dpa/picture alliance

Akizungumza baada ya kupiga kura mjini, Kinshasa, mwanasiasa wa upinzani Martin Fayulu amelalamika dhidi ya kile alichokieleza  kuwa ni kukosekana "utaratibu mzuri" vituoni na kuutuhumu upande wa chama tawala kula njama za kuiba kura.

"Hivi sasa (kambi ya rais) imejiandaa kufanya udanganyifu. Nimewaambia watu wa Kongo, hakuna uchakachuaji safari hii, na kama mtu atajaribu kupora ushindi wetu, ibara ya 64 ya katiba ipo, na tutateremka mitaani kudai ushindi wa umma," alisema Fayulu.

Soma pia: Zoezi la uchaguzi lanedelea DR Kongo

Madai ya dosari vituoni yametolewa pia na wagombea wengine ikiwemo Denis Mukwege na mwanasiasa kigogo Moise Katumbi anayetazamiwa kutoa upinzani mkali kwa Rais Felix Tshisekedi anayewania muhula wa pili.

Zaidi ya wapiga kura milioni 44 wamesajiliwa kushiriki zoezi hilo la kidemokrasia la kumchagua rais, bunge la taifa, mabunge ya mikoa na madiwani.