1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagombea wakamilisha kampeni za uchaguzi wa rais Senegal

22 Machi 2024

Wagombea wa urais nchini Senegal wako katika mikimbio ya mwisho mwisho ya kampeini ya kuwashawishi wapiga kura inayokamilika leo katika kile kinachotajwa kuwa uchaguzi usio wa kawaida.

https://p.dw.com/p/4e2C6
Senegal Dakar
Mmoja wa wagombea urais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye Picha: John Wessels/AFP/Getty Images

Wagombea wa urais nchini Senegal wako katika mikimbio ya mwisho mwisho ya kampeini ya kuwashawishi wapiga kura inayokamilika leo katika kile kinachotajwa kuwa uchaguzi usio wa kawaida baada ya wiki kadhaa za ghasia za kisiasa nchini humo.

Baada ya kujiondoa kwa wagombea wawili mnamo dakika za mwisho, sasa wamebakia wagombea 17 katika kiny'ang'anyiro hicho cha uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili.

Wapia kura milioni 7 wanaruhusiwa kushiriki katika zoezi hilo la kura.

Awali uchaguzi huo wa Rais ulipangiwa kufanyika Februari 25 lakini ukaahirishwa katika dakika za mwisho na rais wa nchi hiyo Macky Sall na kusababisha mzozo mbaya zaidi wa kisiasa kuwahi kushuhudiwa katika muda wa miongo kadhaa .