Jamii ya Wahadzabe ni moja kati ya makabila yaliyobaki duniani yanayoendeleza shughuli za uwindaji, inadhaniwa kuwa jamii hii imeishi tu kaskazini mwa Tanzania, ikila matunda na mizizi, na aina mbalimbali za wanyama kwa miaka 40,000. Katika maadhimisho ya siku ya jamii za watu asilia duniani tunakupeleka kijijini Mang'ola mkoani Arusha kukutana na jamii ya Wahadzabe.