Wahafidhina Austria tayari kuunda serikali na wa siasa kali
6 Januari 2025Matangazo
Siku ya Jumamosi, Kansela Karl Nehammer anayeongoza chama kihafidhina cha OVP alivunja mazungumzo ya kuunda serikali bila ya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia (FPO), ambacho ndicho kilichoshinda uchaguzi wa Septemba kwa mara ya kwanza.
Nehammer alitangaza kujiuzulu ukansela na uwenyekiti wa chama chake, na badala yake, katibu mkuu wa chama hicho, Christian Stocker, amechaguliwa kuwa kiongozi wa mpito.
Soma zaidi: Modi ajadili vita vya Ukraine na Kansela wa Austria
Stocker alisema hapo jana kwamba amepewa idhini na chama chake kuanza mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, kama akialikwa kufanya hivyo.