1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 1,000 wawasili kwenye kisiwa cha Lampedusa

13 Agosti 2023

Karibu wahamiaji 1,000 wamewasili kwenye kisiwa cha Lampedusa nchini Italia tangu Jumamosi, baada ya kuvuka bahari ya Mediterania kwa boti. Watu 270 walipelekwa katika kisicha hicho kwa kutumia meli sita

https://p.dw.com/p/4V7K0
Italien Catania | Migranten am hafen in Catania
Picha: ORIETTA SCARDINO/ANSA/picture alliance

Shirika la habari la ANSA limeripoti kuwa watu 270 walipelekwa pwani kwa kutumia meli sita mapema Jumapili. Wahamiaji hao wanatokea katika mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Ivory Coast, Burkina Faso, Cameroon, Guinea, Nigeria, Senegal na Mali. Inadhaniwa kuwa walianza safari zao kutoka miji ya Pwani ya Tunisia ambayo ni Sfax, Gabes na Mahdia.

Soma pia: Zaidi ya wahamiaji 600 waokolewa Bahari ya Mediterania

Kituo cha kuwapokea wahamiaji hao chenye uwezo wa kuchukua watu 400 kimezidiwa kwa wiki kadhaa na kwa sasa kinawahifadhi zaidi ya wakimbizi 2,000. Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Rome, zaidi ya wahamiaji 96,000 wamefika katika nchi za Ulaya kupitia njia hatari ya kuvuka bahari ya Mediterania kwa mwaka huu, ikilinganishwa na 45,700 waliovuka kwa mwaka mzima uliopita.