Wahamiaji 89 wafa maji Mauritania
5 Julai 2024Shirika la habari la nchi yao limesema kwamba walinzi wa pwani wameipowa miili 89 waliokuwa kwenye mashua kubwa ya uvuvi kwenye ufukwe wa Bahari ya Atlantiki, umbali wa kilomita nne kutoka mji wa kusini magharibi wa Ndiago.
Walinzi hao walifanikiwa kuwaokowa watu wengine tisa wakiwa hai, akiwemo msichana wa miaka mitano.
Soma zaidi: Wahamiaji 11 wafa baharini, 60 hawajulikani waliko
Kwa mujibu wa manusura, mashua hiyo ilikuwa inatokea mpaka wa Senegal na Gambia ikiwa na abiria 170 ndani yake, hiyo ikimaanisha kuwa watu ambao hawajaonekana ni zaidi ya 70.
Ingawa njia ya kutumia Bahari ya Atlantiki ni mbaya zaidi kutokana na mkondo mkali wa maji, lakini watu wanaojaribu kuingia barani Ulaya wamekuwa wakiitumia badala ya Bahari ya Mediterenia yenye ulinzi mkali.