Wahamiaji wapewa uraia wa Tanzania visiwani Zanzibar
5 Septemba 2023Zoezi la kukabidhi vyeti vya uraia kwa wakaazi hao wa Zanzibar,liliongozwa na Rais wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi leo katika viwanja vya Ikulu ya Zanzibar na kuhudhuriwa na watu mbali mbali ikiwemo familia zilizokabidhiwa.Akizungumza kwenye zoezi hilo rais huyo wa Zanzibar amelitaja tukio hilo kuwa la kihistoria.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt Anna Makalala ametoa wito kwa waliokuwa bado hawajajitokeza wajitokeze kujiorodhesha huku akitaka mikoa yote kupewa utambulisho wao.
Wangazija na Wamakonde watambuliwa Zanzibar.
Kwa muda mrefu Wangazija kutoka visiwa vya Comoro na Wamakonde, ambao wameishi nchini tangu kabla ya mapinduzi ya mwaka 1964, wamekuwa wakidai kutambuliwa bila mafanikio, na hali ilikuwa mbaya zaidi mwaka 2018/2019 ambapo walihakikiwa na kunyimwa hati za kusafiria wakiwemo waliotaka kwenda kufanya ibada ya hijja ambapo walipaswa kulipa shilingi milioni mbili za kitanzania. kama anavyobainisha Waziri wa mambo ya ndani, Hamad Masauni.
Soma zaidi:Rais Samia ahitimisha tamasha la Kizimkazi Zanzibar
Itakumbukwa kwamba zoezi la kutowa uraia na kuwatambua watu wasiokuwa na nchi liliwahi pia kufanyika nchi jirani ya Kenya mwaka 2021 nchi hiyo ikiwatambuwa miongoni mwao wato wa jamii ya Shona toka miaka ya 1959 na Wapemba kutoka Tanzania) ambao wameishi Kenya kwa muda mrefu.Kenya iliwapa vitambulisho vya uraia jamii zote hizo.