1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhamiajiUgiriki

Wahamiaji watatu wafa na takriban 25 hawajulikani walipo

23 Septemba 2024

Wahamiaji watatu wamekufa na wengine takriban 25 hawajulikani walipo baada yao mashua yao kuzama hii leo karibu na kisiwa cha Ugiriki cha Samos.

https://p.dw.com/p/4kyds
Ugiriki | Wahamiaji
Ugiriki mnamo Novemba 27, 2021 ilifungua kambi mbili mpya za wahamiaji "zilizofungwa" zilizoshutumiwa na makundi ya kutetea haki za binadamu kwa hatua zake za vikwazo.Picha: Aris Messinis/AFP/Getty Images

Walinzi wa pwani ya Ugiriki wamesema wamefanikiwa kuwaokoa wahamiaji watano wakati shughuli ya utafutaji na uokoaji ikiendelea kwa kutumia meli nne na helikopta huko Agios Isidoros kaskazini-magharibi mwa kisiwa hicho.

Kati ya mwaka 2015 hadi 2016, Ugiriki ilikuwa lango kuu la wahamiaji kutoka Mashariki ya Kati, Afrika na Asia kuingia barani Ulaya, ambapo karibu watu milioni 1 waliwasili kwenye visiwa vya nchi hiyo kwa kutumia mashua.

Mtiririko huo wa wahamiaji ulikuwa umeshuka kabla ya kuibuka tena mwaka uliopita.