1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji zaidi ya 5,000 wakamatwa Libya

4 Oktoba 2021

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa idadi ya wahamiaji waliokamatwa kifani nchini Libya imepindukia watu 5,000, wakiwemo watoto na wanawake, wengi miongoni mwao wakiwa wajawazito, katika ukandamizaji mkubwa..

https://p.dw.com/p/41F0w
NGO I Sea-Watch 3 rettet Migranten
Picha: Darrin Zammit Lupi/REUTERS

Umoja wa Mataifa umesema mhamiaji mmoja alipigwa risasi na kuuawa katika uvamizi huo, ambapo pia watu wengine wasiopungua 15 walijeruhiwa.

Ukandamizaji huo ulianza siku ya Ijumaa katika mji wa magharibi wa Gargaresh, ambao ni kituo kikuu kwa wahamiaji katika taifa hilo la Afrika Kaskazini.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, miongoni mwao 30 walikuwa wajawazito.

Mamlaka za Libya zimeuelezea ukandamizaji huo kama opereshehni ya usalama dhidi ya uhamiaji haramu na ulanguzi wa madawa ya kulevya.