1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahariri wasema Assad ataondoka tu!

Abdu Said Mtullya8 Februari 2012

Damu inaendelea kumwagika nchini Syria hasa baada ya Rais Assad kuimarishwa na kura za turufu za Urusi na China kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na ziara ya Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov.

https://p.dw.com/p/13zCx
This image taken from video filmed over the past several days by an independent cameraman and made available Tuesday Feb. 7, 2012 shows an injured man leaving hospital being helped by friends on the street in the Bab Amr neighbourhood of Homs, Syria. The bombardment of Homs, the hot bed of the resistance to President Bashar Assad's regime, has intensified over recent days, after Syria's allies Russia and China vetoed a Western and Arab-backed resolution at the United Nations that would have condemned the Assad regime's crackdown on dissent and called on him to transfer some of his powers to his deputy. (Foto:APTN/AP/dapd)
Mauaji yaendelea SyriaPicha: AP

Gazeti la "Financial Times Deutschland linasema ziara ya Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alipokewa kwa shangwe kubwa sana nchini Syria. Lakini mhariri wa "Financial Times" anatilia maanani kwamba Waziri huyo alipokewa na watu wa Assad. Na anasema itafika siku ambapo bendera ya Urusi itatiwa moto nchini Syria.Siku ambapo Assad hataweza tena kuwadhibiti wapinzani, licha ya kupewa silaha na Urusi.

Gazeti la "Lübecker Nachrichten" linasema ni mzaha ulioje kwa Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Lavrov kusema kwamba,tamko la Rais Assad kuwa atakomesha mauaji ni hatua ya mafanikio! Gazeti hilo linaeleza kwamba sababu ya Urusi kumuunga mkono Assad ni kutaka kuwa na ushawishi wa kisiasa katika Mashariki ya Kati.Pia Urusi inajaribu kuyasahihisha makosa yake iliyoyafanya wakati wa harakati za mapinduzi katika nchi za Kiarabu.

Mhariri wa gazeti la "General Anzeiger " anasema ingawa mazingira ya Rais Assad wa Syria ni tofauti na ya Gaddafi, Assad pia ataondoka siku moja. Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kuwa Rais Assad anazo turufu nzuri zaidi, na siyo tu kwa sababu Umoja wa Mataifa ulishindwa kupitisha azimio. Sababu muhimu ni kwamba wapinzani hawana nguvu kubwa, na majenerali bado wanamuunga mkono Rais huyo. Lakini kiongozi anaewauwa watu wake kila siku, hatakuwa na mwisho mwema.

Gazeti la "Rhein-Necker"linatilia maanani kwamba mambo hayajakuwa mazuri nchini Libya au Misri baada ya mapinduzi, lakini kwa jumla watu katika nchi za kiarabu wameonyesha kuwa wamechoshwa na udikteta.
Wakati damu inaendelea kumwagika nchini Syria, hapa nchini Ujerumani, jasusi wa Assad amekamatwa. Juu ya kadhia hiyo, gazeti la "Braunschweiger " linasema.

Umoja wa Mataifa bado unapaswa kufanya bidii ya kupata azimio ili uweze kujenga imani upya duniani.Wakati huo huo zipo njia za kuwaimarisha wapinzani nchini Syria, lakini siyo kwa kuwapa silaha bali kwa kuwapa vifaa vya mawasiliano, kama vile simu na kamera.Vifaa hivyo vitawawezesha kuuandaa upinzani vizuri zaidi na pia vitawawezesha kuyaorodhesha mauaji yanayofanywa na utawala wa Assad. Ni kwa njia hiyo kwamba itawezekana kuwakomoa majasusi.

Mwandishi:Mtullya Abdu

Deutsche Zeitungen:

Mhariri:Othman Miraji