Waislamu wanasherehekea Eid wakati mapigano yakiendelea Gaza
16 Juni 2024Siku nne kuu za kusherehekea siku kuu hio inayofanyika kila mwaka katika mwezi wa kiislamu wa Dhul Hijja ambako mahujaji wa kiislamu wanakusanyika katika mji Mkuu wa Makka kwa ibada maalum inayofikia kilele chake baada ya ibada ya Arafat.
Katika hotuba ya Idd, Imamu katika msikiti wa mji mtakatifu wa Makka Sheikh Abdel-Rahman al-Sudais, ametoa wito wa kuwaunga mkono watu wa Palestina.
Ibada ya Hajj yakamilika na kukaribisha sherehe za Eid Ul Adha
Kauli ya Al-Sudais imekuja wakati Marekani mshirika wa Saudi Arabia ikijaribu kushinikiza mpango wa kurekebisha mahusiano kati ya taifa hilo na Israel.
Israel imekuwa ikivurumisha mabomu mjini Gaza tangu wanamgambo wa Hamas waliposhambulia kusini mwa Israel na kusababisha mauaji ya watu 1,200 hali iliyoanzisha mapigano makali kati ya Israel na kundi la Hamas katika ukanda wa Gaza.