1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WAJITOLEA KUHUDUMIA KOMBE LA DUNIA 2006 UJERUMANI.LEO NI FINALI YA KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA KATI YA ENYIMBA YA NIGERIA NA ETUOLE DU SAHEL YA TUNESIA NA MFUMO MPYA WA KOMBE LA KLABU BINGWA AMERIKA KUSINI:

3 Desemba 2004
https://p.dw.com/p/CEHK

MICHEZO

Kombe la Dunia 2006 nchini Ujerumani likianza kupiga hodi,kiasi cha watumishi wa kujitolea 20,000 wamejiandikisha kusaidia katika huduma na shughuli mbali mbali.Hii imewafanya waandazi wa Kombe hilo chini ya mwenyekiti Franz Beckenbauer kuwa na yakini kwamba watajipatia kikosi cha watumishi 15.000 wa kujitolea wanachohitaji 2006.

Idadi kubwa ya vijana wanaozungumza lugha mbali mbali za kigeni wamejiandikisha.Waandazi wamefichua pia kwamba mkongwe mmoja aliezaliwa 1927 ni miongoni mwa waliomba kusaidia.Kombe la dunia nchini Ujerumani litaanza Juni 9 na kumalizika kwa kumtawaza bingwa mpya Julai 9.Kundi hilo la wasaidizi litakua na jukumu kabla na wakati wa changamoto za kombe la dunia kuzihudumia timu 32 ,waheshimiwa-VIPs na waandishi habari na kusaidia pia katika usafiri na mawasiliano ya simu.

Waandazi wa kombe la dunia, wanasaka pia kikosi cha watu wa kujitolea 2000 kwa mashindano yajayo Juni 2005 ya Kombe la mashirikisho hapa Ujerumani-litakalofungua pazia la Kombe la dunia 2006.

Leo jumamosi ni duru ya kwanza ya finali ya kombe la klabu bingwa barani Afrika kati ya Enyimba ya Nigeria na Etoile du Sahel ya Tunisia.

Funali hii inachgezwa katika mji wa sousse,kwenye mwambao wa pwani wa Tunisia.

Enyimba lakini inacheza leo bila ya nahodha wake Uga Opara kwavile alionywa mara 2 na rifu.

Duru ya pili ya kukata na shoka kuaamua hatima ya kombe hili la klabu bingwa mwaka huu itakua Abuja,Nigeria,wiki 1 baadae.

Tunisia, imetangaza kuanzishwa kwa Ligi ya akina dada kwa jicho la kushiriki kwa timu ya dimba ya wasichana wa Tunisia katika Olimpik 2008.

Ligi hii ya wanawake katika ulimwengu wa kiarabu itakua na timu 12 kwa muujibu wa chama cha mpira cha Tunisia.Timu zitaania kombe la shirikisho la dimba la Tunisia.Halafu kuna mpango wa kuanzisha timu 2 za wanawake za Taifa-moja chini ya umri wa miaka 19 na nyengine ya taifa.Azma ni kukata tikiti kwa changamoto za kombe la Afrika la mataifa la wanawake 2007 na Olimpik mwaka unaofuatia.Shirikisho la dimba la dunia FIFA lina timu 2 za wanawake kutoka ulimwengu wa kiarabu kati ya orodha nzima ya timu 117 za akina mama.

Al-Ittihad ya Saudi Arabia, imeibuka klabui bingwa ya bara la Asia .Al-Ittiohad ilibomoa Seongam Chunma mabao 5-0 na kufuta matokeo ya duru ya kwanza ya mabao 3-1.

Tukigeukia Amerika Kusini,huko kuna azma ya kuanzisha mfumo mpya wa kinyan'’anyiro cha Kombe la Amerika Kusini-maarufu Libertadores Cup.Kuna mpango wa kulipanua Kombe hili kuingiza timu zaidi.

Timu 38 -–bili zaidi kuliko zilizoshiriki mwaka jana tena kutoka nchi 11 za Ameruika Kusini zitashiriki katika Kombe hili la klabu bingwa.Mwaka huu Kombe hili limeenda bila ya kutrazamiwa kwa Caldas ya Columbia.Kuongezwa kwa idadi ya timu kuna maana kwamba, Brazil na Argentina kila moja itatoa timu 5 wakati mataifa 8 yaliosalia ya Amerika Kusini yatachangia timu 3 kila moja.

Mexico ambayo imekuwa tu ikialikwa kushiriki,sasa itachangia pia timu 3.

Ama kuhusu mfumo wa jinsi gani timu za Amerika kusini zitakata tiketi zao kushiriki katika kombe la sdunia la FIFA,bado hakuna uamuzi.hii inafuatia kuachana na mfumo wa Ligi uliozusha mabishano na kuzikera klabu za Ulaya zenye wachezaji kutoka Brazil.

Shirikisho la dimba la Amerika Kusini(CSF) limearifu kwamba kuna mawazto mbali mbali pamoja na hayo kutumia mashindano ya Kombe la Amerika Kusini-Copa America kama chombo pia cha kuwachagua waakilishi wa bara hilo kwa Kombe la dunia.Mpango mwengine ni kuzigawa timu katika makundi 5.

Mabingwa wa dunia Brazil wamekuwa wakiukosoa mfumo wa sasa wa kuchagua waakilishi ambamo timu hucheza hadi mechi 18 kati ya Septemba 2003 hadi Oktoba mwakani 2005 kabla kuibuka washindi.

Chini ya mfumo huu timu 4 za usoni katika orodha ya timu za kanda hiyo zitakataa moja kwa moja tiketi zao za kuja Ujerumani kwa Kombe lijalo la dunia 2006.Timu ya 5 inabidi kucheza na timu kutoka eneo la Oceania kabla kuchukua nafasi ya 5 ya Amerika kusini katika Kombe la dunia.

Al Hilal ni mabingwa wapya wa Sudan kufuatia ushindin wao jana wa mabao 2-1 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Al-Merreikh.

CAPS UNITED ililitia kati ya wiki hii ilitawazwa mabingwa wapya wa zimbabwe walipotia kikapuni taji la dimba la zimbabwe kufuatia ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Kwekwe Cables.Mshambulizi wao Leonard Tsipa pekee alitia mabao 4.Hili ni taji la 3 la ubingwa kwa klabu hii ya Harare.

Katika ringi ya mabondia,bingwa wa wa dunia wa taji la WBC,Vitali Klitschko,anajiandaa kwa changamoto yake ya Desemba 11 kati yake na Danny williams huko Las Vegas,Marekani.

Hatahivyo, Vitali klitschko alieishi na kufanya mazowezi yake hapa Ujerumani na Marekani,mawazo yake yako nyumbani Ukraine.Kufuatia uchaguzi wa kutatanisha, klitschko anamuungamkono kiongozi wa upinzani Viktor Yuschenko anaedaiwa amep0okonywa ushindi.

Matokeo hasa ya mvutano bado s wazi ikielekea uchaguzi mpya utrafanywa baadae na kufuta matokeo ya uchaguzi wa majuzi.Atakacho klitschko ni kuona matakwa ya wapiga kura wengi wa Ukraine yaheshimiwe.

Kwa upande wake lakini anaelewa changamoto ya desemba 11 ni muhimu sana tangu kwake hata kwa waukraine.