Wajumbe katika mkutano mkuu wa chama cha CSU humu nchini wamemchagua kwa asili mia 97 bwana Stoiber aendelee kukiongoza chama hicho
3 Septemba 2005Matangazo
Kiongozi wa chama cha kihafidhina cha Christian Social Union Edmund Stoiber amechaguliwa hii leo,mnamo siku ya pili ya mkutano mkuu wa chama chake aendelee kukiongoza chama hicho.Mtetezi huyo aliyeshindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2002 amejikingia asili mia 97 ya kura.Akiwahutubia wajumbe mkutanoni,Bwana edmund Stoiber amemshambulia moja kwa moja kansela Gerhard Schröder na kuzikosoa sera za chama cha Social Democratic.Edmund Stoiber anakiongoza chama hicho kidogo cha CSU tangu mapema mwaka 1999.Vyama ndugu vya CDU/SU vinapigiwa upatu kuwa na nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi uchaguzi mkuu utakapoitishwa september 18 ijayo.