1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajumbe wa Qatar waanzisha tena mazungumzo kuhusu Gaza

24 Oktoba 2024

Wajumbe wa Qatar wameanza tena mazungumzo na kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas baada ya mauaji ya kiongozi wake, Yahya Sinwar, wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4mCEA
Waziri wa Mambo ya nje wa Qatar Blinken na Mohammed bin Abdulrahman Al Thani
Qatar imesema mazungumzo mengine kati ya Misri na wanamgambo wa Kipalestina nayo yanaendeleaPicha: Nathan Howard/Reuters/AP/picture alliance

Waziri Mkuu wa Qatar, Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al Thani, pia amesema mazungumzo mengine  kati ya Misri na wanamgambo wa Kipalestina nayo yanaendelea.

Pia waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, ametowa mwito kwa mara nyingine kwa kundi la Hamas na Israel kufikia makubaliano. Baada ya kukutana na wasuluhishi wa Qatar, Blinken amewaambia waandishi habari kwamba wasuluhishi katika mgogoro huo, wa Mashariki ya Kati watakutana siku chache zijazo kuhusu suala la kufikiwa makubaliano ya kusitisha vita Gaza.

Wakati huo huo, shirika la ulinzi wa rais katika Ukanda wa Gaza, limesema limeshindwa kutowa huduma kaskazini wa Gaza baada ya jeshi la Israel kutishia kushambulia kwa mabomu na kuuwa wafanyakazi wake.