1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Wakazi wa mji wa Kupiansk, Ukraine waagizwa kuhama eneo hilo

16 Oktoba 2024

Mamlaka nchini Ukraine imeamuru kuhamishwa kwa watu katika mji mmoja mkuu na maeneo mengine matatu kaskazini mashariki mwa Kharkiv hapo jana huku vikosi vya Urusi vikisonga karibu na maeneo.

https://p.dw.com/p/4lqTn
Shambulizi la Urusi dhidi ya miundo mbinu ya kiraia mjini Kupiansk, Ukraine mnamo Agosti 9, 2024
Shambulizi la Urusi mjini Kupiansk, UkrainePicha: Ukrainian emergency service

Agizo hilo lilihusisha eneo la Kupiansk, lenye vituo vingi vya reli kando ya Mto Oskil, pamoja na mji wa Borova, ulioko katika eneo la kusini karibu na mji wa Izium.

Akizungumza kupitia televisheni ya taifa, gavana wa eneo laKharkiv Oleh Syniehubov, alisema agizo hilo la kuhamishwa watu ni la lazima.

Syniehubov ameongeza kuwa changamoto kubwa zaidi iko katika eneo la Kupiansk ambapo hawawezi tena kuhakikisha kurejeshwa kwa umeme na huduma za maji kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara.