Wakenya watakiwa kupima kisukari mapema
14 Novemba 2017Matangazo
Kenya ina vituo vitatu vya ubora wa hali ya juu vilivyoanzishwa kupambana na ongezeko la ugonjwa wa kisukari. Vituo hivi, vipo katika hospitali kuu katika miji ya Mombasa, Nakuru na Kakamega. Ugonjwa wa kisukari ambao unazidi kuwaathiri watu wengi hasaa kufuatia mabadiliko katika hali ya maisha, haujapokea hamasisho kubwa ukilinganishwa na magonjwa mengine hasa yanayoambukizwa. Katika maadhimisho ya mwaka huu ya ugonjwa wa kisukari, wito unatolewa kwa watu kujipima mapema ili kuudhibiti na kuepuka athari za ugonjwa huu ambazo hujitokeza baadaye. Mwandishi wetu Wakio Mbogho kutoka Nakuru na taarifa zaidi.