1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMsumbiji

Wakili wa mgombea mkuu wa upinzani Msumbiji auawa kwa risasi

19 Oktoba 2024

Wakili wa aliyekuwa mgombea mkuu wa upinzani kwenye uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 9 nchini Msumbiji, Venancio Mondlane, ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Maputo hii leo.

https://p.dw.com/p/4lzG6
Mgombea wa urais nchini Msumbiji Venâncio Mondlane  baada ya kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka huu nchini humo
Mgombea wa urais nchini Msumbiji Venâncio Mondlane Picha: Romeu da Silva/DW

Wakili huyo, Evino Dias, aliuawa pamoja na mgombea mwingine, Paulo Guambe, wa chama cha Podemos kinachomuunga mkono Mondlane.

Mashahidi wanasema watu wawili wenye silaha walilifyatulia risasi gari la wawili hao lililokuwa limeegeshwa kwenye barabara katikati mwa mji huo mkuu.

Soma pia:Maandamano yaitikisa ngome ya upinzani Msumbiji

Kiongozi wa chama cha Podemos, Albino Forquilha, amethibitishia vifo hivyo kwa shirika la habari la AFP huku chama cha mawakili nchini humo kikilekezea kushtushwa na mauaji ya Dias.

Uchunguzi wa mauaji umeanzishwa

Polisi inasema uchunguzi umeanzishwa lakini haikuthibitisha mara moja utambulisho wa watu hao wawili waliouawa.

Umoja wa Ulaya umetoa taarifa ya kulaani mauaji ya Dias naGuambe na kutoa wito wa uchunguzi kamili na wa wazi utakaowawajibisha wale waliohusika na uhalifu huo.