1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CIA na Mossad kukutana na Waziri Mkuu wa Qatar kuhusu Gaza

Sylvia Mwehozi
27 Oktoba 2024

Wakuu wa mashirika ya ujasusi ya Marekani na Israel ya CIA na Mossad, wanakutana hii leo na Waziri Mkuu wa Qatar mjini Doha, kwa ajili ya mazungumzo ya usitishaji mpya wa muda mfupi wa mapigano katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4mHmY
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinek alipokuwa ziarani Doha
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinek alipokuwa ziarani DohaPicha: Nathan Howard/AP/picture alliance

Wakuu wa mashirika ya ujasusi ya Marekani na Israel ya CIA na Mossad, wanakutana hii leo na Waziri Mkuu wa Qatar mjini Doha, kwa ajili ya  mazungumzo ya usitishaji mpya wa muda mfupi wa mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Afisa mmoja aliye na uelewa wa mazungumzo hayo amelieleza shirika la habari la Reuters, akisema wakuu hao pia watajadili juu ya suala la kuachiwa mateka ambao bado wanashikiliwa na kundi la wanamgambo la Hamas, kwa sharti la Israel kuwaachia pia wafungwa wa Kipalestina.Blinken aelezea matumaini ya kufikiwa makubaliano ya kusitisha vita Sudan

Chanzo hicho kimesema lengo kubwa la mazungumzo ni kuzishawishi pande zote mbili kufikia mwafaka wa kusistisha vita huko Gaza kwa angalau mwezi mmoja, kwa matumaini ya upatikanaji wa kudumu wa makubaliano ya kusitisha vita. Maelezo ya namna au ni mateka na wafungwa wangapi wataachiwa hayakuwekwa wazi.