Walinda amani wajeruhiwa katika mapigano mashariki mwa DRC
18 Machi 2024Askari wanane wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamejeruhiwa kwenye mapigano hayo.
Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo, Bintou Keita, amesema askari mmoja amejeruhiwa vibaya sana katika shambulio la mjini Sake lililotokea Jumamosi. Mji huo wa kimkakati upo kilometa 20 magharibi mwa Goma, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.
Watu walioshugudia wamesema mapigano yalizuka tena katika eneo hilo siku ya Jumamosi. Na kufikia mchana wa Jumapili, hali ya utulivu ilikuwa imerejea katika mji huo.
Chanzo kimoja cha usalama kimeeleza kwa shirika la habari la AFP kwamba askari wa Umoja wa Mataifa walijeruhiwa, wakati mabomu mawili ya waasi wa M23 yalipotua kwenye kambi yao katika wilaya ya Mubambiro mjini Sake.
Kwa habari zetu zaidi tembelea chaneli yetu ya YouTube: